Used Soma Quran for Android?
Developer’s Description
Tarjama hii imeandaliwa kwa lengo la kuwawezesha wazungumzaji wa Kiswahili kufahamu maana sahihi ya Qur-aan Tukufu, nayo ni ya kwanza ya aina yake kwa kuwa inaendana na manhaj ya Nabiy wetu Muhammad ( ) na Salafus-Swaalih; Maswahaba ( ), Taabiiyn na waliowafuata kwa ihsaan mpaka Siku ya mwisho.
Kuna mambo mengi yanayoimaizi Tarjama hii kulinganisha na Tarjama zingine za Kiswahili. Kati ya mambo hayo ni:
Imezithibitisha Sifa za Allaah ( ) zinazolaikiana na Utukufu Wake kama Alivyojithibitishia Yeye Mwenyewe na kuthibitishiwa pia na Rasuli Wake ( ) kama Sifa ya Uluww (Kuweko juu), Istiwaa, Kusikia, Kuona, Mikono, Kuzungumza na Sifa nyinginezo zilizothibiti bila kuzifanyia ta'twiyl (kuzipinga, kukanusha uwezekano), wala tamthiyl (kumithilisha, kulinganisha), wala takyiyf (kuainisha; namna gani), wala tahriyf (kupotosha na kubadilisha maana), kama vile inavyojulikana katika Aqiydah ya Ahlus Sunnah wal Jamaaah..
Imethibitisha masaail yote yahusianayo na mambo yaliyofichika (ghayb) kama Waumini kumwona Rabb wao Siku ya Qiyaamah na Peponi. Pia adhabu ya kaburi, Asw-Swiraatw (Njia ya kuvuka watu Siku ya Qiyaamah), Al-Miyzaan (Mizani) na mengineyo yaliyotajwa kwenye Qur-aan Adhimu.
Tumechagua kwa uangalifu mkubwa misamiati inayowafikiana na makusudio ya Aayah.
Tumefafanua baadhi ya vipengele vinavyohitajia kufafanuliwa kama masaail ya ki-Aqiydah na kadhalika.
Tumeweka sababu za kuteremshwa baadhi ya Aayah au Suwrah na mafunzo yanayopatikana.
Tumetaja An-Naasikh (kinachofuta) na Al-Mansuwkh (kinachofutwa) pale tulipoweza.
Kazi yoyote ya mwana Aadam bila shaka haikosi kasoro, nasi kwa Tawfiyq ya Allaah tumejitahidi kiasi cha uwezo wetu kuepuka hilo. Tunamwomba yeyote atakayegundua kosa, au kasoro, au mponyoko wowote ndani ya Tarjama hii, asisite kutujulisha haraka awezavyo, nasi tutashukuru kwa hilo. Atujulishe kupitia barua yetu pepe: somaqurani@gmail.com
Tunamwomba Allaah ( ) kwa Fadhila Zake, Ukarimu Wake, Upaji Wake, na Ihsani Yake, Atutakabalie kazi hii, hakika Yeye ni Mpaji Mno na Mkarimu Mno.
Explore More

IQuran Pro Plus
Free
The Complete Works of St. Augustine
Paid
Libgen Aurora - Library Genesis
Free
Tamil Quran
Free
CML AIRBUS
Paid
Fire New Guide For Free_Fire 2019
Free
Guide For FileLinked Codes Premium 2020 Pro
Free
How To Write A Biography
Free
VRChat Cute Girl Avatars
Free
The Book of Enoch
FreeFind A Grave
Free
And Then There Were None By Agatha Christie
Free